Serikali ya Korea Kusini imetangaza kufutiliwa mbali mazoezi ya kijeshi ambayo yangehusisha matumizi ya silaha, katika kisiwa kilichoshambuliwa na wanajeshi wa Korea Kaskazini wiki iliyopita.
Jeshi la nchi hiyo limesema mazoezi hayo ni sehemu ya mazoezi ya pamoja yanayoendelea kati ya nchi hiyo na Marekani.
Hata hivyo hakuna sababu yoyote iliyotolewa kuhusu sababu zilizosababisha harakati hizo za mazoezi ya kijeshi zifutiliwe mbali.