Takriban watu sita wameripotiwa kufa nchini Ivory Coast Jumatatu iliyopita wakati wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji katika mji mkubwa zaidi, Abidjan.Walioshuhudia wanasema
wanajeshi watiifu kwa kiongozi aliye madarakani, Laurent Gbagbo, waliwapiga risasi wafuasi wa Alassane Ouattara, kiongozi wa upinzani anayetambulika na jamii ya kimataifa kama aliyeshinda uchaguzi wa urais wa mwaka uliopita.
Ujumbe wa Muungano wa Afrika unaozuru Ivory Coast unatarajiwa kurudia matakwa yao kumtaka Bw Gbagbo ajiuzulu Ivory Coast.