Kumetokea mlipuko mkubwa katika afisi za kampeni za chama cha upinzani nchini Nigeria katika jimbo la Bayelsa lililoko katika eneo la Niger Delta.
Hata hivyo hakuna ripoti zozote za majeruhi.Msemaji wa chama cha Labour Party amesema kuwa chama chake hakitatishwa na fujo zinazotokea.
Mwezi uliopita magenge ya watu waliokuwa na silaha waliwauwa wafuasi wa chama hicho cha Labour katika mkutano wa kampeni.
Hata hivyo, msemaji wa serikali wa jimbo la Bayelsa amesema chama cha Labour Party ndicho kilicho tekeleza mashambulio hayo, ili kuvutia macho ya vyombo vya habari.
Uchaguzi wa urais, bunge na magavana utafanyika Aprili mwaka huu.
0 Comments