Waandamaji nchini Bahrain wakiwa wanafanya Ibada ya maombi baada ya kupigwa kwa mabomu ya machozi na kurushiwa risasi hewani na polisi kwa kuwazuia waisiandamane.Maelfu ya watu waliandamana kuipinga serikali iliyopo madarakani,huku zaidi ya watu 50 wakijeruhuwa,kina mama na watoto na wanaume wengi walikimbizwa hospital ya Salmaniya kwa matibabu zaidi.Msaidizi mkuu wa hospitalini hapo Dr Ali Ebrahim alieleza kuwa majeruhi wengi waliopelekwa hospitalini hapo walikuwa wakivuja damu nyingi toka kichwani,vifuani na kuna wengi waliokuwa wamevunjika.
0 Comments