Watu walikuwa wengi sana,na waliandamana kwa nidhamu ya hali ya juu,hapakuwa na matusi wala kashfa kwa serikali.
 Wananchi walijitokeza na kupendezesha maandamano yao kwa kushika bendera za chama chao,na wenye umoja wa watu wenye pikipiki walishirikiana vyema kujipanga na kuendesha pikipiki zao kwa mbwembwe barabarani jiji Mwanza.
 Mwenye Bango alilinyanyua juu ili lionekane kwenye vyombo vya habari,mwenye nyimbo aliimba ili mradi asikike na kuondoa dukuduku lake la siku nyingi ndani ya nafsi yake.
Bwana Freeman Mbowe mmoja wa kiongozi mkubwa wa chama cha chadema aliunguruma na kupigiwa makofi sanaaa.aliwaambia wananchi wake kuwa wakti wa ukombozi sasa umefika wananchi waamke.
Viongozi mbalimbali wa chama cha chadema walikuwepo kwenye mbilinge hiyo ya maandamano jijini Mwanza,walioketi hapo kwa nyuma mwenye miwani meusi na skafu ya chadema shingoni ni mwanamuziki mkongwe wa bongofaleva na sasa ni Muheshimiwa Mbunge wa Chadema mkoani Mbeya,Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr Sugu nae alikuwepo katika kuhamasisha chama chake.Kiukweli mkutano ulikuwa wa Amani na Utulivu sana,hakuna aliyelalamika juu ya kuonewa au kusumbuliwa na polisi,na zaidi kiongozi  wa chama hicho bwana Mbowe aliwasifu wana usalama wa Mwanza kwa ushirikiano wao mzuri waliouonyesha katika mkutano huo.