Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amekiambia kituo cha televisheni cha taifa kuwa Osama Bin Laden na wafuasi wake, ndio wa kulaumiwa kwa maandamano yanayotikisa nchi yake.
Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amekiambia kituo cha televisheni cha taifa kuwa Osama Bin Laden na wafuasi wake, ndio wa kulaumiwa kwa maandamano yanayotikisa nchi yake.Wanasiasa wa upinzani na viongozi wa kikabila wamefanya mkutano muhimu katika mji wa mashariki wa al-Badya, kuonesha umoja dhidi ya Kanali Gaddafi.
Kanali Ghaddafi amesema waandamanaji hawana madai yenye msingi, na walikuwa wakiongozwa na kiongozi wa al-Qaeda.

"Bin Laden.... huyu ndio adui anayewadanganya watu. Msidanganywe na Bin Laden," amesema.
"Ni wazi kuwa sasa jambo hili linaongozwa na al-Qaeda. Vijana wenye silaha, watoto wetu, wanachochewa na watu ambao wanatafutwa na Marekani na nchi za Magharibi.
"Wale wanaochochea ni wachache, na hatuna budi kuwakamata."
Amesema vijana hao waandamanaji "wanafurahia kupiga risasi hasa wakiwa wamelewa".
Amesema Libya sio kama Misri na Tunisia, ambazo zimeshuhudia viongozi wao wakiondolewa madarakani, kwa sababu watu wa Libya wana uwezo wa kubadili maisha yao kwa kupitia kamati.