Walianza maandamano kama mzaa vilee!!hawakujua kuwa dola haitaki kabisaa matatizo nchini.Hawa ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Wakiendeleza maandamano kwa nyimbo na kelele nyingi huku wakikimbia mchakamchaka kama wanajeshi vilee...
Wazee wa kazi FANYA FUJO UONE (FFU) kikosi cha kazi kilipotangaza kwa mdomo vijana walifikiri kuwa wanatania,ndipo kazi ya hatua ya kwanza ya kurusha mabomu ya machozi ilipoanza kudhibiti maandamano ya wanafunzi hao chuo kikuu.
Wanafunzi hawakusitita kurudi nyuma pale walipoona kwamba KIKOSI cha kuzuia ghasia kimekamilika ipasavyo,walioweza kukimbia walikimbia utasema kuna mashindano ya mbio,na kuna waliokuwa wakianguka kutokana na kukosa balance kwa jinsi walivyokuwa wakikanyagana kila mmoja aokoe maisha yake.
Hapa ni kwa kumalizia kazi tu na kuweka mipaka kwamba hakuna atakayevuka kwenye moshi huu wa bomu la machozi,Tanzania ni nchi nambari moja katika bara la Africa yenye kusifika kwa amani,na yeyote mwenye kutaka kuivuruga amani kwa njia yeyote huwa hapewi nafasi na kama akigoma chamoto ukiona.
0 Comments