Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amegoma kuondoka madarakani licha ya kuwepo kwa maandamano makubwa ya kupinga serikali, ambayo amesema yamechafua sura ya nchi.Katika hotuba yake kubwa tangu kuanza kwa vuguvugu wiki iliyopita, Kanali Gaddafi amesema dunia nzima inaitazama Libya na kuwa maandamano hayo yana "mhudumia shetani".
Akisoma vifungu kutoka ndani ya katiba ya nchi hiyo, amesema maadui wa Libya watauawa.
Kanali Ghaddafi akizungumza kwa ghadhabu amesema ameleta heshima kwa LIbya. Kwa kuwa hana nafasi yoyote ya kujiuzulu, amesema
atasalia kuwa kiongozi wa mapinduzi.
Amelaumu machafuko hayo kwa "mahasidi na wasaliti" ambao wanataka kuchora taswira ya Libya kama sehemu ya machafuko na "kuwadhalilisha" wananchi wa Libya. Katika sehemu ya hotuba yake amewaita waandamanaji kuwa ni mende au panya au mamluki.
Kituo cha televisheni cha serikali kilitangaza kuwa Kanali Ghaddafi atatangaza "mabadiliko makubwa" katika hotuba yake, lakini jambo pekee katika hilo ni mamlaka kupewa serikali za mitaa.