Habari wapendwa, napenda kuwashirikisha juu ya habari hii ya hawa watoto ili uweze kuona kama unaweza kuwasaidia kwa chochote ulichojaaliwa na Mungu.
 
"Watoto Jackline,Joseph na Johnson ni watoto mapacha waliozaliwa tarehe 22.08.2010 Kihonda Morogoro. mtoto Jackline alizaliwa kwa njia ya kawaida na Joseph na Johnson walizaliwa kwa upasuaji. Uzazi huu ulipelekea mama yao kufariki pindi tu baada ya upasuaji. Wahudumu wa hospital walifikiri kuwazika watoto hawa kwa kuwa hawakulia baada ya kuzaliwa kumbe ni wazima. Ndipo baada ya jirani wa mama wa mzazi huyu (ambaye ni mzazi wa mtoto wa kituoni Tz 811-0163)  kuwa karibu na kukubali kukaa nao hospital Mungu akawapa kupumua na kuendelea kuishi bila ya kulia.
 
Baba mzazi wa watoto hawa alikimbia na hafahamiki aliko baada ya kuona changamoto ya kimaisha.
Mpaka sasa watoto hawa wanalelewa na mama huyu ambaye amejitolea kuwahudumia na kukaa nao ambaye ni mzazi wa mtoto Tz 811-0163. Kitendo hiki cha huruma ya mama huyu cha kuwahudumia watoto hawa tangu hospital hadi hivi sasa  kimesababisha mume wa mama huyu ambaye ni mzazi wa mtoto wa kituo Tz811-0163 kumwacha mama huyu kwa kuona changamoto ya kulea watoto ambao siyo wake.
 
Mpaka hivi sasa watoto hawa wana miezi 6 na wanalelewa na mama huyu kwa kutegemea msaada toka kwa mtoto wake anayemtumia sehemu ya kipato chake na kukitumia kwa bili ya maziwa ya watoto pia.
 
Taarifa zaidi waweza kupata toka kwa mama huyu mlezi wa watoto hawa kwasimu # 0659 193 8 25.(Tigo)
+255 659 1938 25  Mama huyu hana msaada wowote toka serikalini wala taasisi yoyote.
 
Mungu wa mbinguni akupe kufikiri zaidi ya maelezo haya na kuona jinsi ya kufanya sawa sawa na Mungu anavyotubariki.KWA YOYOTE ALIYEGUSWA NA TANGAZO HILI NA MWENYE NIA THABITI YA KUWASAIDIA WATOTO HAWA NA MAMA MLEZI AMBAYE AMEKUBALI KUACHIKA KWA MUMEWE KWA AJILI YA WEMA WA KUWALEA WATOTO HAWA, TAFADHALI AWASILIANE NA MAMA MLEZI WA WATOTO HAO KWA NJIA YA SIMU HAPO JUU...NINAENDELEA KUTAFUTA UWEZEKANO ZAIDI WA KUIPATA ACCOUNT NAMBA YAKE NA ANUANI YA HUYO MAMA MLEZI WA WATOTO HAO ILI IWE VYEPESI KWA WENYE HURUMA NA KUTAKA KUMSAIDIA MLEZI HUYO.(Pichani juu ni picha ya watoto wahusika wenye kuhitaji msaada wowote ili waweze kujikimu na maisha yanayowakabili).
 
MUNGU AWAJAALIE MOYO WA IMANI WATU WOOTE WENYE NIA THABITI YA MSAADA HUO.AHSANTENI.