Watu 11 wamekufa katika mkanyagano kwenye mkutano wa kisiasa nchini Nigeria.Mkutano huo uliofanyika katika mji wa kusini wa Harcourt, ulikuwa sehemu ya mkutano wa kampeni wa rais Goodluck Jonathan, kabla ya uchaguzi wa mwezi April.Pichani ni raisi wa Nigeria bwana Goodluck Jonathan.

Uchunguzi

Watu wengine 29 wanasemekana kujeruhiwa katika mkutano huo, ambao ulifanyika kwenye uwanja wa michezo.
Umati huo ulishituka, baada ya polisi kufyatua risasi hewani, kujaribu kutawanya watu katika milango ya kuingiliwa uwanjani, wakati watu wakitoka, kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo na kukaririwa na shirika la habari la Reuters.
"Kulikuwa na kundi kubwa la watu, na sehemu ilikuwa imejaa," amesema Ken Saro-Wiwa, msaidizi wa Rais Jonathan wa masuala ya kimataifa, ameiambia Reuters.
"Ni mwisho wa kusikitisha katika siku iliyoanza vizuri," amesema Bw Saro-Wiwa.