Mmoja wa washukiwa wa mabomu yaliyotokea Uganda tarehe 11 mwezi wa 2010 mjini Kampala Uganda ambapo watu zaidi ya 70 waliuawa, hatimae yuko mikononi mwa polisi ya Uganda. Mshukiwa huyo ni raia wa Tanzania na amewasili Uganda akitokea Tanzania.
Msako wa polisi ya Uganda kwa ushirikiano na polisi wa nchi jirani pamoja na polisi ya kimataifa Interpool, kuwatafuta walioshiriki na kupanga mashambulio hayo ya ya mabomu unazidi kupata matunda.
Akitajwa kwa jina la Hija Suleman Nyamondondo mwenye umri wa miaka 31 raia wa
Tanzania inasemekana mchango wake katika shughuli hiyo nzima ilikuwa kusafirisha mabomu hayo kuyaingiza Uganda. Hawakusema kuwa aliyatoa wapi lakini imesisitizwa yeye ndie alibeba jukumu la kuzifikisha Uganda. Mwaka jana mkuu wa polisi ya Uganda alikuwa amelalamikia Tanzania imekataa kushirikiana nae kumpeleka kijana huyo nchini Uganda.
Amewasili uwanja wa Ndege wa Entebbe alfajiri ya siku ya Jumanne katika ndege ndogo na kupokelewa na maafisa polisi chini ya ulinzi mkali. Mikono ya Suleman ilikuwa imefungwa pingu na pia minyororo ilifungwa miguuni kwake. Mabomu aliyoleta moja ililipuka katika uwanja wa mchezo wa raga wa Kyandondo, eneo la Lugogo ambapo watu wengi waliuawa jingine katika mkahawa mmoja wa Ethiopian Village mtaa wa Kabalaga.
Kukamtwa kwa mshukiwa huyo kumejumulisha wote kufikia 30 ambao wanakabiliwa na mashataka ya kuua watu 72 na kuwajeruhi wengine wengi katika milipuko ya mwezi wa Julai. Mbali na Waganda kuna Wakenya, Wasomali pamoja na raia wa Pakistan