Majeshi yanayoiunga mkono serikali yamezidi kuwashambulia waasi nchini Libya, nahivyo kuwalazimu kurejea nyuma katika mji wa Bin Jawad.
Mapigano hayo mapya yameibuka baada ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali kukutana mjini London kwenye mkutano wa kujadili mipango ya usoni ya Libya.
Awali Rais wa Marekani Obama alijitetea kwa kufanya uamuzi wa kuidhinisha harakati za kijeshi kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani, akisistiza Marekani imejihusisha kwa kiwango kidogo.
Lakini pia alisema kumwondoa Kanali Gaddafi kwa nguvu ni kosa.
Majeshi yanayompinga Kanali Gaddafi yamesogea sana upande wa magharibi kutoka kwenye ngome yao ya Benghazi katika siku za hivi karibuni- wakisaidiwa sana na mashambulio ya anga ya kimataifa- yakiteka idadi kadhaa za jamii za kipwani na mitambo muhimu ya mafuta, ikiwemo Ras Lanuf, Brega, Uqayla na Bin Jawad.
Vifaru vya kivita vya jeshi la Raisi wa Libya bwana Muammar Gaddafi ambavyo vinafavya mashambulizi ya nguvu iasi kwamba waasi wameanza kurudi nyuma kwa kuzidiwa nguvu.
0 Comments