Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwauliza maswali ya masomo ya Fizikia na Kemia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Edward Lowassa Wilayani Monduli, alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea majengo ya shule hiyo pamoja na kuangalia maendeleo ya wanafunzi hao. Makamu wa Rais yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya siku nne ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo. (Picha na Amour Nassor)