Vyanzo vya usalama vimesema, aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak amepelekwa hospitali huko Sharm el-Sheikh.
Chanzo cha usalama kimeiambia shirika la habari la AFP, " Mubarak alilazwa katika hospitali ya kimataifa Sharm el-Sheikh mchana huu, huku kukiwa na ulinzi mkali kwenye eneo hilo."
Bw Mubarak, mwenye umri wa miaka 82, aliachia madaraka Februari 11 kufuatia maandamano ya siku 18 yaliyopata umaarufu dhidi ya uongozi huo.
Aliripotiwa kuwa na hali mbaya lakini washirika wake walikataa hilo.
Aliitwa na mwendesha mashtaka kuhojiwa juu ya madai ya rushwa na mauaji ya waandamanaji.
Bw Mubarak, watoto wake wa kiume na wake zao wamezuiwa kuondoka nchini humo na mali zao zimepigwa tanji.
Waandishi walisema amekuwa kimya huko Sharm el-Sheikh, kufuatia hatua yake ya kukimbilia katika jumba lake la kifahari baada ya kutolewa madarakani.