Umoja wa mataifa imekanusha taarifa kuwa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo kuwa ameondolewa mjini Abidjan.
"tofauti na taarifa za awali, Laurent Gbagbo bado yuko katika hoteli ya Golf" mji mkuu, msemaji wa Umoja wa mataifa Farhan Haq alisema.
Alikamatwa baada ya makabiliano ya juma zima kutoka kwa majeshi ya mpinzani wake,anayetambuliwa na jamii ya kimataifa kama rais Alassane Ouattara.
Bwana Ouattara ameahidi kuwa Gbagbo hatofanyiwa jambo lolote baya.Bado hakuna usalama Abidjan, na milio ya risasi inasikika kila wakati.
Wakuu wa majeshi waliokuwa wanamuunga mkono Bwana Gbagbo wamekuwa wakitangaza kumuunga mkono Ouattara,lakini kuna taarifa kuwa baadhi ya wanajeshi na wanamgambo wamekataa kujisalimisha.
Karibu watu 1,500 wameuawa kote nchini na wengine milioni moja kukimbia makao yao wakati wa mzozo huo,ulioanza mwezi Novemba wakati Bwana Gbagbo alipokataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa urais ambao alikuwa ameshindwa.