Kiongozi maarufu wa chama cha upinzani nchini Rwanda ndugu Bernard Ntaganda amehukumiwa kwenda jela miaka 4 baada ya kupatikana na hatia ya uchochezi wa mvutano wa kikabila.Mamlaka husika nchini humo imetamka rasmi kuwa bwana Ntaganda amehukumiwa ijumaa iliyopita na kwamba kwa sasa ameanza kutumikia kifungo chake jela.