Wanajeshi katika mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou wameasi, huku milio ya risasi ikisikika usiku kucha.
Uasi huo umeanza wakati baadhi ya walinzi wa rais walipoanza kupiga risasi hewani wakipinga kutolipwa posho za nyumba.
Rais Blaise Compaore(Pichani) alitarajiwa kukutana na mjumbe wa Umoja wa Mataifa mjini humo, maafisa wamesema, baada ya kukimbia usiku mzima.
Mapema, Bwana Compaore, ambaye yuko madarakani tangu 1987, alijaribu kupata namna ya kuwatuliza askari hao baada ya kutokea malalamiko kama hayo mwezi uliopita.
Mwandishi wa BBC Mathieu Bonkoungou akiwa Ouagadougou anasema ghasia hizo zilisambaa katika kambi nyingine za jeshi na upigaji risasi hewani ukaendelea mpaka karibia na alafajiri.
Hata hivyo inaripotiwa kuwa mji huo mkuu umetulia sasa.
Maandamano yalifanyika siku ya alhamis katika mji huo mkuu na kwenye miji mingine kupinga kupanda bei ya vyakula na shutuma nyingine za kuvunjwa kwa haki za binadamu, shirika la habari la Ufaransa-AFP limeripoti.
0 Comments