May Day ni sikukuu ya Wafanyakazi Duniani,kila mfanyakazi ana haki ya kupumzika leo hii.
Mkoani kwangu kuna baadhi ya wafanyakazi waliopita na mabango wakiandamana kuhusu,baadhi ya wafanyakazi kupoteza kazi zao,mishahara yao midogo na kukosa ajira.
Watoto wengi wamejumuika viwanjani kucheza michezo pamoja,leo ni burudani kila kona kwani kila mmoja amepumzika nyumbani.
Japo ni siku ya mapumziko kwa wafanyakazi,ila mashindano ya magari yanaendelea kuwapa watu burudani kama kawaida.
Wazee kwa vijana hupendelea kujifurahisha kwa mazoezi,pichani kama unavyowaona wakilenga shabaha za mishale.mapumziko ya leo ni burudani kila pembe.
0 Comments