Watu wawili wameuawa na wengine kujeruhiwa vibaya kusini mwa mji wa Antwerpen baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana,Watu hao waliopigwa risasi inasemekana ni raia wa Albania,kwa mujibu wa shahidi aliyeona tukio zima alisema"Tukiwa ndani ya Pub tulisikia milio ya risasi,na ile kuchungulia nje tukaona kinamama wamelala chini na wengine wakiwa wanakimbia hovyo barabarani,baada ya muda tukagundua kuna watu wameshauana.Polisi walipofika eneo la tukio,wakapata maelezo kuwa walikuwa ni gangstars raia wa Albania ambao walikuwa na ugomvi wao tokea siku za nyuma.hata hivyo polisi walisema watatoa ripoti kamili baada ya uchunguzi kukamilika. Inasemekana idadi ya raia toka Albania inazidi kuwa kubwa kwa matukio ya mauaji nchini Belgium.
0 Comments