Wanawake wa Kisomali wakiwa wameshikilia picha ya rais wa Uganda Yoweri Museven na bendera ya nchi yao kumuomba rais Museven kuendelea kuyaacha majeshi yake nchini Somalia ili kuilinda amani ya serikali ya mpito iliyopo madarakani hivi sasa.Maandamano hayo yalifanyika karibu kabisa na Ikulu ya rais mjini Mogadishu nchini Somali.
Muda mfupi baada ya maandamano kulitokea mlipuko wa ghafla na kuwafanya watu wakimbie hovyo,hata hivyo Rais Museven aliwahakikishia watu wa Somali kuwa atawaongezea mwaka mmoja tena ili kuilinda amani inayowekwa na umoja wa Afrika nchini humo.
0 Comments