Rais Sarkozy na Chansela Merkel wamekubaliana Ugiriki ipewe mkopo mwengine

Viongozi wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro wanakutana mjini Brussels hii leo kutafuta namna ya kukabili tatizo la madeni linalokumba serikali za ulaya.
Viongozi hao pia watajadili mkopo wa pili kwa Ugiriki kufuatia mpango wa mkopo wa dola bilioni 150 ulioidhinishwa mwaka uliopita.
Hata hivyo kuna wasiwasi kuwa huenda mgogoro huu wa kiuchumi unaenea kwa mataifa mengine kama vile uhispania na Italia.

Serikali ya ugiriki inahitaji msaada zaidi ilikuweza kulipa madeni yake.
Ilitarajiwa kuwa baada ya hatua ya kwanza ya kuisadia nchi hiyo, uchumi wake utaimarika kiasi kwamba wataweza kuomba mikopo ya kujisitiri kutoka mashirika ya fedha kwanzia mwaka ujao lakini hili huenda lisifanyike.
Kutokana na hali hii viongozi wa bara ulaya wanakubaliana kuwa juhudi zaidi zinahitajika kuisadia nchi hiyo.
Mpango ni kuwa Ugiriki utapata mkopo zaidi kutoka majirani wake na pesa zingine zitapatikana baada ya kuuzwa kwa baadhi ya mali za serikali.
Huku viongozi wa ulaya wakijiandaa kwa mkutano wa leo pia kumetolewa pendekezo kuwa benki za ulaya zililipia kiasi fulani cha kodi ambacho kitakumika kuisaidi ugiriki na nchi zingine zenye matatizo ya kiuchumi.
Mkutano wa leo ukilinganishwa na ule uliofanyika mwezi uliopita safari hii soko la fedha nchini Uhusipania na Italia linakabiliwa na shinikizo kali tofauti na kipindi kilichopita.
Madeni ya nchi hizo ni makubwa zaidi ukilinganisha na yale ya Ugiriki, Ureno na Ireland, nchi ambazo zinapokea msaada kutoka umoja wa ulaya.
Kufuatia hali hii nchi wanachama wa umoja wa ulaya sasa wanahimizwa waongeze michango yao kwenye mfuko maalum wa kunusuru nchi zinazokabiliwa na matatizo ya kiuchumi.
Ingawa wazo hilo ni zuri bila shaka kisiasa, litapingwa sana hasaa nchini Ujerumani ambapo suala la kutumia pesa zake kufadhili mikopo hiyo linapingwa na raia wa nchi hiyo.