Habari za leo waungwana.!!
Natumai wengi wetu tumejaaliwa afya njema na kwa wale wagonjwa Mungu awajaalie wapone kwa haraka ili waweze kurudi katika taratibu zao za maisha yao ya kila siku.
Waungwana nilikuwa na tatizo la maumivu ya jino kwa siku kama tano hivii siku za nyuma (miezi sita iliyopita) nilijitahidi kujikaza kuona kama nitapata nafuu ila wapi...nilipofika siku ya sita ilinibidi mwenyewe niamke asubuhi na kuelekea hopsital ili kupata suluhu ya jino langu.Nilipofika hospital hawa jamaa zetu wa majuu huwa wana taratibu kwamba hawawezi kukupa tiba bila kuweka appointment labda kama una ugonjwa mkubwa sana au wa dharura.
Nilijaribu kuwaelewesha maumivu ninayohisia na kuonyesha sura ya unyonge zaidi,pale mapokezi kulikuwa na mdada aliyeonyesha kuhisi maumivu yangu,alichofanya ni kuinua mkono wa simu na kumuomba dokta kama itawezekana anipe huduma kwa siku ile.Dokta akamjibu kwamba nirudi baada ya masaa mawili toka muda ule,kwa upande wangu nilihisi kama ni miaka miwili ila sikuwa na jinsi,nilimuonyesha yule dada hali fulani ya kumshukuru kwa kuniombea kwa dokta.nilirudi nyumbani kwa kuwa hapakuwa mbali,hayakutimu hata masaa mawili nilirejea hospitalini pale na kukaa kwenye chumba cha kusubiria ili niitwe na kupata tiba.
Ulipofika muda wangu niliitwa na dokta ambaye alinifuata kweye chumba cha kusibiria (waiting room).Nilipofika mule chumba cha dokta nikamuelezea jinsi ilivyokuwa na maumivu ninayohisi,dokta alichukua mikasi na sindano ya ganzi alinichokora kama dakika kumi na tano hivii.baada ya muda wake kumaliza aliniruhusu na kunisisitiza nisitie chochote mdomoni mpaka lisaa liishe,kwa kuwa ganzi iliisha baada ya muda kama wa dakika 45 hivii nikaanza kuhisi maumivu upyaa tena kwenye meno mengi na sio lile jino moja.nikajikaza nikijua ni mwanzo tu.nililala usiku ule mpaka kesho yake,asubuhi yake nikawa nikibrush meno kwa maji ya baridi nahisi maumivu kwa upande wa ule jino lililokuwa likinisumbua,sasa badala ya kuhisi maumivu ya jino moja nikawa nahisi meno yote yanauma.
Kiufupi dokta alizidisha ufundi ambao sikuhitaji anifanyie vile..Kiukweli mimi na madaktari huwa hatupatani (naogopa hospital) nikawa najikaza tu ili nisirudi tena hospital,ukapita mwezi nikaona acha nirudi tu nikamueleze dokta maumivu na jinsi alivyonitibu sikupendezewa.
Nilipofika na kumueleza dokta alichofanya alinipiga x-ray na kusema meno yapo sawa ila tatizo ninalo mimi,eti sitafuni vizuri,akaniwekea kijiplastic kwenye meno na kuniambia ning'ate kile kijiplastic,nikafuata vile yeye anataka ila haikusaidia kitu. nikakaa tena miezi miwili kurudi tena nikamueleza dokta please naomba chochote ulichoongeza kwenye jino langu ondosha maana sifurahii kabisaa maumivu haya,dokta aliniambia niketi kisha akachukua kifaa kimoja hivii na kuniambia nifungue mdomo,nilifuta nini dokta anasema na alikipachua kijipande fulani hivii toka kwenye jino palepale nikahisi hali fulani ya amani.
Kiukweli mpaka leo bado nina maumivu fulani kwa mbali ambayo sina hata raha nayo ila kurudi kwa daktari yule sitaki tena maana kajua kucheza na meno yangu bila kujali hali ya maumivu yangu.kingine ni kwamba hata nikifikiria daktari mwingine nahisi hali kama itakuwa ni ileile maana nina rekodi mbaya na madaktari wa meno,kuna siku za nyuma pale Magomeni Hospital nilishawahi kungo'lewa jino nilihisi yule dokta anataka kungo'a ubongo au anavuta jicho langu nilipiga kelele kama mtoto aliposimama tu nilimwambia dokta pesa yangu ya gharama za matibabu nimesamehe kwaheri.alijua utani ila sikurudi tena.
Nilipoenda Muhimbili kuna dokta ambaye jina lake la mwanzo nimelisahau ila jina lake la mwisho ni Maganga,tulifanya utani sana kabla ya kunipa matibabu alijihisi kama sisi ni ndugu kutokana na jina la Maganga,kiukweli siwezi kumsahau maana aliningo'a jino bila hata kuelewa kama kashamaliza kazi yake,aliponiambia niinuke sikuweza kuamini maana nihisi bado anaanza matibabu kumbe kashamaliza.
Madokta wa majuu sio wote wanajua kutibu wagonjwa,maana huyu aliyenipa tiba ya jino langu HAKUNITIBU,KANITIBUA.
Maganga One.
0 Comments