MAHARUSI WALIVYOPENDEZA KILA MMOJA ALIWAPENDA,JE WEWE?HONGERA SANA BWANA JIMMY KWA KWELI MLIPENDEZA SANA,KILA LA HERI KATIKA NDOA YENU.
Bwana harusi Jimmy na mkewe Betty wakiwa na tabasamu la nguvu baada ya kukubaliwa rasmi kuwa mke na mume.
Wakipata flash mbili tatu toka kwa camera man amabye ni Maganga One,bwana Jimmy na mkewe wanaonekana watu wenye mvuto machoni mwa watu.
Mawifi wa bibi harusi walikuwepo ndani ya mjengo ili kupata kumbukumbu siku ya furaha.
Mzaa chema mama mzazi wa harusi,mama Betty mwenye bluu akiwa na binti yake katika kumbukumbu ya harusi ya binti yake na mkwewe bwana Jimmy.
Bwana Yusuph kulia akipata picha ya pamoja na dada yake.Yusuph ndiye aliyebeba jukumu lote la kumuozesha dada yake kwa bwana harusi.
Wapambe ambao walihakikisha harusi na maharusi wanapendeza mwanzo mwisho,toka kushoto ni Brondine,bwana harusi,bi harusi na mdogo wa bi harusi Binia.
Watu wa karibu wa mama wa bi harusi walihudhuria katika sherehe za ndoa ya bwana Jimmy na mkewe bi Betty.
Familia nayo inapata picha ya pamoja, ni ndugu,jamaa na marafiki.
Maganga One na maharusi,kwa kweli maharusi walipendeza.
Vijana ambao walitua kwenye harusi mchana kwa ndege ya KLM toka USA kuja kuhudhuria harusi ya bwana Jimmy.
Ulaya ni Ulaya kama unavyoona,siongei sana hao ni marafiki wa karibu sana wa bwana harusi bwana Jimmy.
Yani ni full Maanjumathi..............tulikula,tukarudia na tukafungiwa,kuna waliovimbiwa maana msosi wa nguvu ulitawala ukumbini hapo.
Wasiokuwepo waliitwa kwa njia ya simu,hawa ni vijana waliotua toka Marekani kuja kwenye harusi ya bwana Jimmy.
Toka kushoto ni Dj Kee,bwana harusi na Dj Khatib ambao walihudhuria harusi ya bwana Jimmy.
Mashangazi,madada na mama wa bi harusi wakishangalia vijimambo vilivyokuwa vikichukua nafasi kwenye harusi.
Jimmy na dada yake ambaye alishiriki vyema katika kabisa katika kufanikisha kaka yake anapendeza ile yenyewe.
Mahanjumathi na vinywaji kedekede vilishika nafasi yake ukumbuni.
Kaka James na wapwa wake wa karibu kabisa.
Mapacha ambao hawakubaki nyuma katika kumpa tafu bi harusi,hapo wakipata picha mbili tatu.
Mashoga wa karibu wa bi harusi wakipata kumbukumbu.
Watu wa karibu sana kwa maharusi walikuwepo ukumbini hapo.toka kulia ni brother Moses na kushoto ni ndugu wa karibu wa maharusi hao.
Ndugu,jamaa ma marafiki wa karibu sana walikuwepo ukumbini hapo.
3 Comments