Aliyekuwa makamu wa rais nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jean Pierr Bemba, ametangaza kuwa atawania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Novemba mwaka huu.
Bemba anazuiliwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, kuhusiana na mashtaka ya uhalifu wa kivita.
Bemba ambaye alimaliza katika nafasi ya pili katika uchaguzi mkuu miaka mitano iliyopita, anatuhumiwa kuongoza makundi ya waasi yaliyotekeleza uhalifu wa kivita katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, CAR, kati ya mwaka wa 2002 na 2003.
Wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, mamia ya watu waliuawa wakati wafuasi wa Bemba, walipokabiliana vikali na wafuasi wa rais wa nchi hiyo Joseph Kabila, mjini Kinshasa.