Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Benchmark Productions Ltd inayoendesha shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011 (BSS) Rita Paulsen akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip jijini Dar, kwa madhumuni ya kuwatambulisha wadhamini wapya wa shindano hilo,ambao wanatambua na kuthamini vipaji vya Tanzania,Wadhamini hao ambao pia watahakikisha BSSsecond Chance 2011 inachukua sura mpya kwa Watazamaji.Ritha amewataja wadhamini hao kuwa ni kampuni ya simu za mikononi ya Tigo, PSI (Salama Condoms),CHAMPION (Engender healt),NSSF na Golden Tulip Hotel.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Benchmark Productions Ltd inayoendesha shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011 (BSS) Rita Paulsen akitaja washiriki waliofanikiwa kuingia kumi bora,kama waonekavyo nyuma pichani ambao ni Rogers Lucas (23),Bella Kombo (5),Chibi Dayo (7),Sarafina Mshindo (12),Hajji Ramadhan (11),Mary Banyukwa (15),Mary Lucos (16),Waziri Salum (27),Beatrice William (4) pamoja na Iman Lissu (12).
Pichani washiriki kumi bora waliofanikiwa kuingia kwenye shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011 (BSS) .



0 Comments