Jaji anayeendesha kesi ya aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak amezuia matangazo ya moja kwa moja ya televisheni na kuamuru kesi hiyo kusikilizwa kwa pamoja na waziri wake wa zamani wa mambo ya ndani Habib al-Adly.
Bw Mubarak mwenye umri wa miaka 83, anakabiliwa na hukumu ya kifo kama atakutwa na hatia ya kuamuru mauaji ya wandamanaji katika machafuko ya kisiasa mwanzoni mwa mwaka.
Mara hii tena aliletwa mahakamani akiwa kwenye kitanda cha hospitali, akizungumza na watoto wake Alaa na Gamal. Jaji alipata shida kurejesha utulivu, na kuwageukia upande wa utetezi kuleta ushahidi.
Alaa na Gamal pia wako kesi. Wanakana mashataka ya ufisadai.
Bw Mubarak aliong’olewa madarakani na mamia ya waandamanaji mwezi Februari.
Kesi yake inayowahusu pia watoto wake wawili Alaa na Gamal, iliahirishwa mpaka Septemba 5.
Makundi ya watu wanaomuunga mkono na wapinzani wake yaligombana nje ya mahakama huku wengine wakikasirishwa na uendeshaji wa kesi kwenye televisheni.
Madai ya Tantawi
Mamia ya polisi wa kutuliza ghasia walishika doria nje ya mahakama siku ya Jumatano.
Wafuasi kadhaa wa Mubarak walikusanyika baadhi yao wakipiga kelele "Ni Mmisri mpaka kifo" na "Hosni Mubarak si Saddam". Mapigano yalikuwa yakizuka mara kwa mara na watu wanaompinga Mubarak.
Helkopta ya Jeshi ilitua katika eneo la mahakama, ikiwa imembeba Bw Mubarak. Televisheni ya Taifa ilimuonesha Rais wa zamani akiwa amevaa suti ya blue, akiwa amebebwa kwenye gari la wagonjwa juu ya kitanda cha hospitali. Mtoto wake Alaa alijaribu kuizua Kamera.
Mahakamani , Jaji anayeendesha kesi hiyo Jaji Ahmed Refaat aliuliza iwapo upande wa utetezi walikuwepo, akianzia na Bw Mubarak, kisha vijana wake wawili.
Baada ya mapumziko mafupi Jaji Refaat aliamuru kesi hizo zisikilizwe pamoja mwezi ujao.
Alitangaza kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya televisheni "kwa faida ya umma " na kuahirisha kesi mpaka Septmeba 5.
Wachambuzi wanasema uamuzi huo utarahisisha kazi ingawa wapinzani wa Bw Mubarak nje ya mahakama walionekana kukasirishwa.
Mmoja wao Sherif Mohamed, ameliambia shirika la Habari la Reuters: "Ni upuuzi, mwelekeo wa kesi ni muhimu kwa umma. Kutokuonyesha moja kwa moja kwenye televisheni ni kukubaliana na Mubarak."
0 Comments