Mwakilishi wa Televisheni ya Emmanuel ya The Synagogue Church Of All Nations, Martha Harvey akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete mkoba wenye Sh milioni 25 kwa ajili ya waathirika wa ajali ya meli ya mv Spice Islanders iliyozama na kusababisha vifo vya mamia ya watu hivi karibuni. Mchango huo uliokabidhiwa Ikulu, Dar es Salaam, ulitolewa na Kiongozi wa Kanisa hilo, Nabii Themitope Balogun Joshua, ambaye anaishi makao makuu ya kanisa hilo Lagos, Nigeria. (Picha na Freddy Maro).