A for Antwerpen....hii herufi unaikuta katika stesheni ya treni pale Antwerpen,nilijaribu kuizungu vizuri ile stesheni kiukweli ni kubwa sana kiasi kwamba kama si mtulivu basi utajikuta unaliza wapi pa kutoka wapi pa kuingilia.Nilijaribu kutafuta hata kipande cha karatasi kwa kweli sikuweza kuona uchafu.
Stesheni hiyo sio tu kwa wasafiri bali kila mmoja anayejisikia kutalii utamkuta pale amejituliza,ama kwa kukaa na kutazama au ameshikilia kamera yake na kuflash mapicha.Kama si maandishi yangu au macho yangu ebu thibitisha na wewe kwa kuiangalia hiyo sakafu je kuna hata kijikaratasi?
Kingine kwamba wazungu wanapenda sana Starehe,mzungu anafanya kazi na pesa yake upendelea kuitumia kufurahisha nafsi yake.Kwenye mtaa mmoja unaweza kukuta bar hata 25 na zote zimejaa watu kwenye viti. 
Usafi wa mji sio tu kwamba yawe maghorofa,Miji ya wenzetu neno miti kwa kweli wanalipa kipaumbele sana,miti ikiioteshwa vizuri na kupangwa kwa mistari hupendezesha muenekano wa mji kuwa mzuri sana.Unaweza kujikuta mahakamani na hata kulipa faini pesa nyingi sana kisa kukata mti.