Mapigano yametokea kusini mwa Somalia,ambapo ndege za Marekani zisokuwa na rubani pamoja na wanajeshi wa serikali, wameshambulia wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema vijiji vitatu karibu na bandari ya Kismayo vilishambuliwa kwa mabomu kutoka angani.

Bandari ya Kismayo ni muhimu kupitisha bidhaa za maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji.

Inaarifiwa kuwa ndege moja ya Marekani ilidunguliwa na al-Shabaab wanasema wanayo wao.

Huku nyuma, wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na wanamgambo, wanaarifiwa kupambana na al-Shabaab kaskazini zaidi, katika eneo la Gedo.

Maelfu ya Wasomali wamekimbilia mji wa Garbahare, unaodhibitiwa na serikali, kuepuka njaa.