Mwandishi mmoja wa Uganda amewashutumu Polisi kwa kumpiga na kumtishia kumuua baada ya kumweka korokoroni kutokana na kitabu chake kumhusu Rais Yoweri Museveni.

Vincent Nzaramba ameiambia BBC kuwa alizuiliwa kinyume cha sheria kwa siku tano kwa kuchapisha kitabu kinachojulikana kama "People Power - Battle the Mighty General".

Msemaji wa Polisi alisema kuwa Bw Nzaramba alihojiwa kwa uchochezi.
Mwaka huu Uganda imekabiliwa na mfululizo wa maandamano dhidi ya utawala wa miaka 25 wa Rais Yoweri Museveni.

Nzaramba amesema Polisi walimkamata Jumamosi baada ya kuisaka nyumba yake katika mji mkuu wa Uganda Kampala na kutaifisha chapa za kitabu chake, komputa ya mkononi na simu.


Ushawishi wa Gandhi


alihojiwa kuhusu kitabu chake, msemaji huyo aliongeza kusema hii sio mara ya kwanza wao kumkamata mtu kwa kumiliki nyaraka za uchochezi.

Nzaramba aliiambia BBC kuwa anashuku kama Polisi wamesoma kitabu chake, ambacho kina picha ya Rais Museveni akiwa na sare ya kijeshi na maandishi yanayosema "Amekwisha" yakiwa chini ya picha hiyo.

Msemaji wa Polisi Judith Nabakooba alithibitisha kuwa Nzaramba, ambaye aliachiwa huru Jumatano