Gaddafi hajulikani alipo
Katika ripoti yake mpya, shirika hilo linasema kuwa pamoja na kuwa vikosi vinavyomuunga Gaddafi ndiyo vimehusika na ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu, wapiganaji wanaompinga pia wamehusika katika mauaji na kutesa watu.
Mapema,Muammar Gaddafi alisisitiza katika ujumbe kupitia televisheni kuwa wataendelea na mapigano hadi "wapate ushindi".
Kwa sasa haijulikani kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 69 yuko wapi.
Waasi walipata upinzani mkubwa
Habari zaidi zinasema kuwa, kiongozi wa baraza la mpito la Libya Mustafa Abdul Jalil ametoa hotuba yake ya kwanza kwa taifa mjini Tripoli tangu walipomuondoa Gaddafi, akitoa wito wa kuwa na taifa lenye msingi wa demokrasia ya kiislamu yenye mfumo wa ''kadri''.
Vikosi vinavyompinga Gaddafi vimesitisha mashambulio yake dhidi ya mji wa Bani Walid ambao unadhibitiwa na vikosi vinavyomuunga mkono Gaddafi. Waandishi wa habari wanasema walipata upinzani mkubwa kinyume na walivyotarajia.
0 Comments