Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dr. Sander Gurbuz (kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa mashine 10 za kutunzia watoto wachanga waliozaliwa kabla ya muda, ambapo amesema kuwa nchi yake inathamini mchango wa Tanzania na hatua mbalimbali inazochukua katika kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaozaliwa na wale walio chini ya umri wa miaka 5 ikiwa ni katika kutimiza Malengo ya maendeleo ya Milenia. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TPM Mining and Energy Bw. Burak Buyuksarag.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dr. Haji Mponda (Kulia) akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ambapo ameishukuru Serikali ya Uturuki kwa msaada huo na kwa kuthamini mchango wa Tanzania katika kutimiza malengo ya Milenia likiwemo la kupunguza vifo vya watoto wachanga. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Afya ya Uzazi na mtoto Dr. Neema
RusibamayilaBaadhi ya mashine hizo zilizokabidhiwa na Serikali ya Uturuki kwa Tanzania.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dr.Sander Gurbuz (kushoto) akikabidhi kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Mponda msaada wa moja wapo kati ya mashine 10 za kutunzia watoto wachanga waliozaliwa kabla ya muda zenye thamani ya shilingi milioni 50 ambazo zitapelekwa katika hospitali mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.
0 Comments