Sura zilizojaa furaha leo hii jijini Amsterdam,Bwana Harusi akionyesha furahakuwa na mkewe.bwana harusi ni ndugu Habibu na bi harusi ni bi Monica.harusi iliyopendeza na kufanya ilifungwa msikiti wa Ya Tayyba mjni Amsterdam nchini Holland.(picha zote na Maganga One Blog).
Waawwoow...!!! Kuoa au kuolewa raha jamaniii,Hongereni maharusi ama hakika mmependeza.
Imam wa msikiti wa Ya Tayyba jijini Amsterdam ambaye aliifungisha ndoa ya bwana Habibu na bi Monica leo hii.
Kutokana na furaha na mawaidha kumuingia vilivyo bwana harusi,hakuweza kuvumilia na kuanza kuangusha kilio,kiukweli mawaidha yalikuwa ni mazuri yenye msisitizo wa kuachana na dunia na kufanya kazi za kumfurahisha Mwenyezi Mungu.
Kutoka kushoto mwenye fulana ya mistari ni bwana  Abba ambaye alihudhuria harusi ya leo,na kulia mwenye fulana nyeusi ni Kamanda Kaseke walikuwa makini kusikiliza mawaidha mazuri kutoka kwa Imam wa msikitini hapo palipofungishwa ndoa hiyo.
Wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali walikuwepo kushuhudia harusi hii ya bwana Habibu.
Kila harusi lazima iwe na mashahidi na kama mnavyojionea mashaidi wakiendelea kusikiliza mawaidha.
Kwa picha ya pamoja ili kumpongeza bwana harusi,kutoka kushoto ni Chura,Kabila,bwana harusi Habibu,Pacha,Bachala na Halili.hawa ni marafiki,makaka wa karibu wa bwana harusi.
Kazi na dawa,yani full misosi kila mmoja ilipofika wakati wa msosi alipata sahani iliyojamaa kila unachokijua.
Kulia ni Aunt Jamillah akipata Flash kama kumbukumbu na maharusi wetu leo hii.
Kila mmoja alipata kumbukumbu na maharusi wetu leo hii.kiukweli walipendeza sana maharusi hao.
Wageni waliotoka jiji la LONDON kuja kushuhudia harusi ya bwana Habibu na bi Monica walikuwepo ukumbini hapo na kupata picha kama kumbukumbu na maharusi wetu.
Kila mmoja alipendeza pale ukumbini,kulia ni kaka wa bi harusi ambaye alitoka nchini France na kuja Holland kushuhudia harusi ya dada yake Monica akifunga pingu ya maisha na bwana Habibu.

Bwana Hussein Chura kulia akipata picha na maharusi wetu leo hii kama kumbukumbu kwamba nae alikuwepo katika ndoa hii nzuri ya leo.
Ndugu,jamaa na marafiki wakipata picha za pamoja na maharusi wetu leo hii ukumbini hapo.
Waacha weeee,jamani kupendwa rahaaaaaaa.........bi Monica akimwambia mumewe kwamba wao ni kuzama,kuzuka mpaka kufa.
Bidada Fatma aliyesimama nyuma na mzee wetu na kulia na  aliyekaa mwenye shati la drafti ni Pacha wakipata picha ya pamoja na maharusi wetu leo hii.
Wera weraaaa kuanzia leo huyu ni mke halali wa bwana Habibu,Hongera bi Monica umependeza kisawasawa.
Yes....Kuanzia sasa wewe ni mume halali wa bi Monica,huyu ni bwana harusi ndugu yetu Habibu,kiukweli kapendeza sana  na mavazi yake ghali yaliyotoka mbali.
Watoto ni ishara ya Amani na Upendo...kuwepo kwao kwenye harusi hii ni ishara tosha kuwa ndoa ya bwana Habibu na Bi Monica itakuwa na Amani na Upendo maishani.Maganga One Blog inawatakia kila la kheri maharusi hawa,Mungu awazidishie kila lililo jema na maisha yenye vizazi vyema insh`Allah....Amen.(picha zote na Maganga One Blog.