Kocha mkongwe wa mchezo wa ngumi , Habibu KInyogoli (kulia) akimwelekeza jinsi ya kutupa masubwi bondia Issa Sewe wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Dar es salaam jana Sewe anajiandaa na mpambano wake na Ramadhani Shauli litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu.(picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com)
Mbunge wa Ilala Mussa Zungu atashughudia ZAIDIya mabondia 42 wanatarajia kushiriki katika mashindano ya mchezo wangumi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba16 mwaka huu Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha wa Klabu ya Ashanti ya Ilala,Rajabu Mhamila, 'Super D' alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwakushirikisha Klabu 12 kutoka katika maeneo mbalimbali.
Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.
Super D alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuhendelezakuhamasisha mchezo wa ngumi nchini ikiwa ni pamoja na muendelezo wamchezo huo unanaofanywa na Kinyogoli Foundation.
“Tumeandaa mashindano ya ngumi ambayo yatashirikisha vijana mbalimbalina lengo letu ni kuhamasisha mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuuendelezaili uweze kutuletea faida hapo baaye” alisema.
Kocha huyo alisema kuwa vijana watakaoshiriki watakuwa katika uzito mbalimbali kuanzia Unyoya mpaka uzito wa juu.
Alisema kuwa pia wanatarajia kushirikisha mabondia wa kike kutokakatika klabu hizo hizo Aliongeza kuwa katika mapambano hayo mgenimwalikwa ni Mbunge wa Ilala Mussa Zungu ambaye kwa mara ya kwanzaatangalia mchezo huo ukipigwa katika jimbo lake
Aliongeza kwa kusema kuwa wanaitaji wadaumbalimbali wajitokeze kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya vijana ikiwemomaji kwa ajili ya mchezo huo kwa siku hiyo wenye nia ya kutaka kusaidiaau kushiliki kwa kuchangia chochote wanaweza kuja katika ukumbi wamazoezi uliopo Amana Ilala au kufika Ashanti Boxingi clabu kwamawasiliano zaidi unaweza kuwa siliana na Kocha Mkongwe, HabibuKinyogoli kwa simu 0655928298 au unaweza kuwasiliana na Super D BoxingCoach O713,0787-406938 Email.superdboxingcoach@gmail.com wadaumbalimbali mnakalibishwa.