Kikosi cha kagera Sugar ambacho leo hii kimeikubali Yanga African kwamba walistahili kuitwa mabingwa.
Golikipa wa Kagera Suga, Hannington Kalyesubula akioko moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake mbele ya beki wa Yanga, Nadir Canavaro Kagera Sugar

Furaha ya ushindi huwa haichagui ufanye nini...yani kinachokuja akilini ndicho kinapewa nafasi,Pichani vijana wa Yanga wakiselebuka kwa furaha baada ya kuifunga timu ya Kagera Sugar kwa goli moja leo uwanja mpya jijini Dar es Salaam.Mzee wangu Mzee Said wa Ilala Dar unaona kazi ya vijana wa Jangwani?
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Dar Young Africans wakipata picha kabla ya kuingia uwanjani na kuwaadhibu vijana wa Kagera Sugar kwa goli 1-0 katika uwanja wa Taifa mpya jijini Dar es Salaam.