Denmark imekuwa nchi ya mwanzo duniani kutoza kodi ya shahamu -- kodi zaidi dhidi ya vyakula venye shahamu nyingi, ambayo inaonekana kuwa inadhuru.
Siagi, maziwa, jibini, nyama, mafuta na vyakula vilivotengenzwa na mafuta, vitatozwa ushuru ikiwa vitakuwa na mafuta zaidi ya asili-mia mbili pointi tatu ya mafuta yaitwayo "saturated fat", ambayo mara nyingi inatokana na nyama na maziwa.
Kwa mfano bei ya siagi itapanda kwa kama dola moja na nusu kwa kilo.
Watu wamekuwa wakinunua vyakula hivo akiba ili kuhepa kodi hiyo.
Jumuiya ya wazalishaji chakula na vinywaji, inasema watu wa Denmark watavuka mpaka kwenda kununua bidhaa hizo nchi nyengine.
Baadhi ya wanasayansi wanaona vinavofaa kulengwa zaidi ni chumvi, sukari, na unga mweupe kuwa ndivyo vinavodhuru afya zaidi.
0 Comments