Mrembo aliyetwaa taji la mkoa wa Mtwara mwaka huu, 'Miss Mtwara 2011', Rahma Swai,(pichani) amefariki dunia jana asubuhi katika hospitali ya mkoa wa Mtwara ya Ligula, imefahamika.
Taarifa zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam jana, zilieleza kuwa mrembo huyo amefariki dunia kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.
Ilielezwa zaidi kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa mrembo huyo kutoka Mtwara na kuupeleka Changanyikeni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi zilikuwa zikiendelea.
"Ni kweli mrembo huyo amefariki na taratibu za kumleta Dar es Salaam zinaendelea, huko Mtwara alikuwa chuoni na ndiko alikoamua kushiriki mashindano ya urembo mwaka huu," alisema mmoja wa wadau wa sanaa hiyo ambaye alikataa jina lake kutajwa gazetini.
Baada ya kutwaa taji la mkoa wa Mtwara, marehemu Rahma aliuwakilisha mkoa huo katika mashindano ya Kanda ya Mashariki ambayo hushirikisha pia mikoa ya Lindi, Morogoro na Pwani lakini hakufanikiwa kufika fainali za taifa zilizofanyika Septemba 10 jijini Dar es Salaam na mrembo wa Ilala, Salha Israel, kuibuka mshindi. 
Marehemu Rahma (kushoto) enzi za uhai wake,Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi ..Ameen.habari zaidi ingia Nipashe.