Wulff tayari amekutana na Rais Hamid Karzai wa Afghanistan, kwanza alikuwa na mazungumzo na watetezi wa haki za binadamu hususan wale wanaopigania haki za wanawake kwa ajili ya maandalizi ya mkutano kuhusu Afghanistan uliopangwa kufanyika mjini Bonn Ujerumani hapo mwezi wa Desemba.
Hapo mwezi wa Mei mwaka jana, mtangulizi wa Wulff ambaye alikuwa Horst Köhler alivitembelea kwa muda mfupi vikosi vya Jumuiya ya Kujihami vya NATO vilioko kaskazini mwa Afghanistan lakini hakukutana na Karzai.
Matamshi yaliotolewa na Köhler kwamba uwekaji wa vikosi vya Ujerumani nchini Afghanistan unaweza kuwa na maslahi ya kiuchumi kwa nchi hii,yalisababisha kujiuzulu kwake. Ujerumani ina zaidi ya wanajeshi 5,000 waliowekwa nchini Afghanistan. Ziara ya mwisho rasmi iliofanywa na mkuu wa nchi wa Ujerumani nchini Afghanistan ni ile ya Rais Heinrich Lubke hapo mwaka 1967.
0 Comments