BAADA ya zile dawa za Kichina za kuongeza makalio, ‘hips’ na matiti zilizotikisa Bongo na kubainika kubeba madhara makubwa kama vile ‘kalio’ moja kuwa kubwa kuliko lingine, kujazia zaidi chini kuliko juu na mwili kufa ganzi, zilikosa soko, lakini sasa zimeibuka nyingine za kienyeji, Ijumaa lina ripoti kamili.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kupitia kwa wataalam mbalimbali wa tiba za asili Bongo, ulibaini kuwa dawa hizo zimejaa tele kwa waganga wa kienyeji.
Ilifahamika pia kuwa hivi sasa dawa hizo zinachangamkiwa na wanawake ile mbaya wakiamini kwamba hazina madhara kama zile za Kichina.
NI MCHANGANYIKO WA MITI 60
Mmoja wa wataalam hao aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutochorwa jina gazetini ili kutoharibu ‘biznesi’ yake hiyo alisema kuwa, dawa hiyo ni mjumuisho au mchanganyiko wa miti zaidi ya 60 inayopatikana kwenye misitu mikubwa hasa mikoani.
INAITWAJE?
Ijumaa lilipotaka kujua jina la dawa hiyo, mtaalam huyo alisisitiza: “Nimeshakuambia ni mchanganyiko wa miti zaidi ya 60, haina jina isipokuwa mteja akifika anatakiwa aseme kama anataka ‘mzigo’ wa ‘saizi’ gani.”
UNACHAGUA KALIO UNALOTAKA
Mtaalam huyo alikwenda mbele zaidi na kuweka kweupe kuwa dawa hiyo ni kiboko ya Mchina kwani dozi na bei yake hutegemea aina ya kalio analolitaka mteja husika.
“Ukitaka dogo, la kati au kubwa, kila moja lina dozi na bei yake ‘so’ inategemea mteja amechagua la aina gani,” alisema mtaalam huyo.
WATAALAM WA TIBA ASILIA WANASEMAJE?
Baada ya kukusanya data za kutosha, Ijumaa lilifanya mahojiano na wataalam mbalimbali wa tiba za asili ambapo walikuwa na haya ya kusema:
MJUKUU WA BABU
Mganga maarufu kwa jina la Mjukuu wa Babu anayepatikana Mwananyamala jijini Dar es Salaam alifunguka:
“Nakwambia hii dawa ni kiboko ya zile za Kichina. Ni dawa nzuri na kusema kweli watumiaji ni wengi. Ni mchanganyiko wa miti zaidi ya sitini ambao huwa unatoa aina moja ya dawa.
ZAWAVUTIA MASTAA
“Tatizo baadhi ya waganga wanashindwa kuwa nayo kwa sababu hawana uwezo mkubwa wa kuifahamu miti husika, mimi ninayo na nimeshawapa mastaa kibao wa Kibongo hasa wa Kinondoni, wametumia na wengi wao imewavutia.”
Ijumaa lilipotaka listi ya mastaa wanaokwenda kwa mganga huyo na ambao wameonesha mabadiliko, Mjukuu wa Babu alisema: “Siyo utaratibu wetu kuvujisha habari za wateja wetu ‘so’ mtanisamehe kwa hilo.”
MASTAA WATOA USHUHUDA
Huku akiwa na mshtuko kusikia mastaa wanatumia, ‘vuvuzela’ wetu aliwainulia mkonga wa simu ambapo kila mmoja alitoa ushuhuda wake;IRENE UWOYA:
“Sina uhakika na dawa yoyote ya kuongeza makalio kwani sijawahi kutumia na wala sina shoga aliyetumia ili kuthibitisha, kwanza ya nini? Kama huna, huna tu!”
JANETH ISINIKA:
“Nawaonea huruma sana wanawake wenzangu wanaohangaika na dawa za kukuza makalio, mimi naona kuwa mtu anayefanya hivyo basi ajue anaishi kwa kutegemea wanaume hivyo anatengeneza makalio awakamate kirahisi.”
KAJALA MASANJA:
“Siamini kama kuna dawa za kienyeji za kukuza makalio, ni uongo mtupu, ya nini kuhangaika? Kama Mungu amekunyima, amekunyima tu.”
BADRA:
“Sikubaliani na matumizi ya hizo dawa, kwanza ni kumkosoa aliyekuumba, utamsikia mtu anaapa kabisa kwa Mungu kuwa lazima awe kama mimi, Wema au Kajala na kweli baada ya muda unamuona amebadilika, mwisho afya yake inabadilika kwa kuwa ameilazimisha kuliko uwezo wake.”
AGNES MASOGANGE:
“Kinachowaponza ni kuhadaika na umbo langu, hili umbo si la Kichina wala mganga wa kienyeji, ni kitu ‘orijino’ kutoka tumboni kwa mama, isitoshe kwa hapa Bongo sidhani kama utaalamu huo wa kuwa na dawa hizo za kukuza makalio upo, watu wasidanganyike na picha zinazochorwa kwenye mabango ya matangazo ya waganga, ni kuvutia wateja tu.”SHILOLE:
“Aku! Mimi sijawahi kutumia dawa ya kuongeza kalio, langu ni la urithi kutoka kwa bibi yangu. isitoshe kwa Mnyamwezi ni jambo la kawaida kuwa na wowowo.”
AUNT EZEKIEL:
“Kama kuna watu wanatumia hizo dawa nawaonea huruma, nahisi hawayafahamu madhara yake kwani ni makubwa sana.”
SINTAH:
“Mimi najua hizo dawa zinapatikana China, kwa hapa Bongo sidhani kama zipo, kuhusu za kienyeji, ni kama yale yaliyotokea Loliondo.”
SAUDA MWILIMA:
“Mwanamke lazima ujiamini kutokana na ulivyoumbwa, siamini kabisa kama kuna dawa ya kienyeji inayoweza kubadilisha maumbile ya mtu.”
LULU:
“Sina ‘komenti’ kwa hilo kwani sifahamu chochote, mimi ‘mgeni’ hapa Bongo.”
ZILISHAPIGWA MARUFUKU
Miezi kadhaa iliyopita, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ilitangaza kupiga marufuku dawa za Kichina kutokana na kubainika kuwa na madhara makubwa kwenye maumbile ya mwanadamu.
0 Comments