Jk akisalimia na makamu mwenyekiti wa ccm bara Mh:Pius Msekwa na anayefuata ni Waziri mkuu Mh:Mizengo Pinda.
Jk alisalimia na viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi.
Unajua nini mzee? sogea kidogo nikwambie basiii,eeehee...!!! Heshima haichagui mkubwa au mdogo,Rais wa Tanzania akiinamisha kichwa kusikiliza neno la kijana.Je wewe unayesoma una heshima za kusikiliza watoto?
Rais Jk akisalimiana na mbunge wa Chadema Mh: John Shibuda,pamoja na upinzani wanaoleta Chadema kwa Ccm ila bado tunashukuru kwamba fair play ipo na Amani nchini tunayo Mungu awabariki viongozi wetu wote,wawe wa chama tawala na hata wa upinzani.
Mzee mzima Jk akisalimia na viongozi wa chama.
Na Mwandishi Maalum, Dodoma, Jumamosi Nov. 19, 2011.
Baada ya mapumziko mafupi katika Ikulu ndogo ya Dodoma Dkt Kikwete alielekea ukumbi wa St. Gaspers ambako aliongea na wabunge wa CCM na kupata nao chakula cha usiku.
Katika hotuba yake, Dkt Kikwete aliwapa changamoto wabunge hao wa CCM waende kwa wapiga kura wao na kuwaelemisha kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya uliopitishwa Jumamosi Bungeni Dodoma.
Dkt Kikwete aliwasisistizia wabunge hao umuhimu wa kupeleka elimu hiyo ya mchakato wa kupata katiba mpya kwani hivi karibuni kumekuwepo na upotoshaji mkubwa wa nini kinachoendelea, na kusema kuwa wakiwa wabunge wa chama tawala ni wajibu wao kuelimisha umma kwamba kanuni na sheria zote zimefuatwa katika kupitisha muswada huo ambao umesomwa kwa mara ya pili, baada ya kusomwa mara ya kwanza kwa mujibu wa sheria.
Rais Kikwete aliwakumbusha wabunge hao kwamba mchakato huo si jambo geni na kwamba ndio uliofuatwa na Marais wote toka wa awamu ya Kwanza hadi ya tatu, akisisitiza kwamba ni muhimu wanancho wote wakaelewa hilo, ikizingatiwa kwamba kuna baadhi ya watu wachache wanaotaka kupotosha umma kwamba hatua hiyo ni batili wakati sio kweli, ikizingatiwa kwamba kila lililo katika katiba ya sasa limezingatiwa.
Pia aliwasihi Watanzania kujitokeza kutoa maoni yao ya ni katiba gani wanayoitaka pindi muda wa kufanya hivyo utapowadia, na wasikubali kughiribiwa na wachache waliopania kupindisha ukweli.
Kwa mujibu wa ratiba leo Jumapili kutakuwa na Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ukumbi wa White House kitachofanyika kutwa nzima, kitachofuatiwa na kikao cha Kamati kuu ya CCM Jumatatu na Jumanne. Halmashauri kuu ya CCM itakutana kuanzia Jumatano hadi Ijumaa.

0 Comments