Binti Maganga One akiwa amepozi kusubiri wapambe waje washuhudie upulizaji wa mishumaa na ukataji wa keki.
Una miaka mingapi? soma vidole hivyooooooo ...
Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa uhai huu nilionao leo hii,napenda kuwashukuru wazazi wangu wawili kwa malezi wanayonipa,napenda kuwashukuru ndugu na jamaa zangu wote wa karibu kwa mchango wao wa ushauri juu ya maisha yangu.
Ujumbe kwa watoto wenzangu kwamba,Tuwaheshimu wazazi,Tusome kwa bidii kwani dunia ya sasa inapokwenda kama huna elimu mbele kiza kinene,kingine napenda kutuna salam zangu duniani kote kwa watoto wenzangu na wale wote wanaonifahamu.Nawapenda sana.Binti Maganga hakutaka kuzimiwa mishumaa bali aliinamisha shingo na kuipuliza kwa kasi na mishumaa yote ikazimika,kila mmoja akampigia makofi ya kumpongeza kwa siku yake ya kuzaliwa.
Kwa furaha na heshima alianza kumlisha keki mzazi wake.
Akaomba nae alishwe keki yake.
Akamlisha mdogo wake Roshan.
Akamlisha mdogo wake Laila.
Akamlisha Aunt yake mama Laila.
Laila kushoto,mama Laila na binti Maganga.
Binti Maganga akiwa na Anko wake ambaye ni mwakilishi wa Maganga One Blog nchini Holland,shekh Hija ambaye alikuja kushuhudia sherehe za anko wake akikata keki na kuzimisha mishumaa.
Binti Maganga akiwa na mama yake na mdogo wake akilishwa keki.
4 Comments
Wako
James
Mwajy