Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima lilloko Kawe Tanganyika Pakers akimkaribisha Dk Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na Naibu Waziri wa Ujenzi katika ibada iliyofanyika jana kwenye kanisa hilo na kuhudhuriwa na Waziri wa Afrika Mashariki mzee Samwel Sitta na baadhi ya wabunge kadhaa, Mzee Samwel Sitta amesema Mwakyembe amekwenda kanisani hapo ili kutoa ushuhuda kuhusu ugonjwa wake kwa ujumla ambapo FULL SHANGWE ilishuhudia tukio hilo. Dk. Harrison Mwakyembe ametoa ushuhuda akimshukuru mungu kwa kumbariki na kuendelea kumpa nguvu juu ya afya njema, Mwakyembe ambaye alikuwa amevalia kofia na Glovu katika mikono yake, ameongeza kwamba tangu alipokuwa ameondoka kwenda nchini India kwa matibabu Oktoba 9 mwaka jana hakuwahi kuvaa viatu, lakini jana amevaa, hivyo akamshukuru mungu kwa miujiza yake. 
Dk. Harrison Mwakyembe wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge, kushoto ni Mbunge wa Same Mashariki Mama Anne Kilango Malecela, Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta na Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli. 
Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli kushoto , akizungumza na Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa ibada hiyo jana. 
Harrison Mwakyembe akishuka katika madhabahu mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo jana.