Mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea hivi sasa jijini Kampala nchini Uganda kwa wafanyabiashara kugomea kuendelea na shughuli zao za kazi kutokana na benki kuu nchini Uganda kuongeza riba kubwa kwa benki za wafanyabishara.
Eneo la New Tax jiji Kampala likiwa na umati wa watu wakiwa ambao walikuwa wakifuatilia kujua hatma ya wafanyabiashara hao kuhusu mgomo wao.
Maduka mengi jijini Kampala yalikuwa yamefungwa kwa kuonyesha msisitizo wa mgomo huo.Hakukuwa na fujo haina yoyote mgomo ulikuwa wa amani na usalama.
Baadhi ya wananchi waliathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na mgomo huo,kwani wengi walikosa mahitaji yao muhimu ya kila siku.
Mpaka mchana wa jana hali iliendelea kuwa kama unavyojionea pichani,hakuna duka lililofunguliwa, 
mazungumzo yanaendelea leo baada ya jana wafanyabiashara kukutana na rais museveni na wawakilishi wa mabenki. (Picha zote na Daniel wa Maganga One Blog Kampala).