HUDUMA za usafiri wa reli ya kati kwenda katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa zirejea rasmi Julai mwaka huu baada ya kuwasili kwa vipuri vilivyoagizwa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kukarabati wa kichwa cha treni ya abiria.
Kichwa cha treni hiyo chenye namba 8818, kiliharibika takribani miaka mitatu iliyopita na kusababisha huduma za usafiri wa reli kwenda katika mikoa hiyo.Habari kuhusu mpango wa kurejesha huduma hizo, ulitangazwa juzi na Meneja wa Karakana Kuu ya Reli ya Kati iliyoko mjini Morogoro, mhandisi Ngoso Ngosomwile.
Mhandisi huyo alikuwa anawasilisha taarifa yake kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athumani Mfutakamba, aiyetembelea karakana hiyo.
Meneja hiyo alisema vipuri hivyo viliagizwa tangu mwishoni mwa Desemba mwaka jana na kwamba zoezi la kuvisuka upya huenda likachukua miezi sita wakati matengenezo yakitarajiwa kudumu kwa mwezi mmoja zaidi.
Ngosomwile alisema tayari serikali imekabidhi fedha zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati na matengenezo ya injini na mabehewa ya treni.Kwa upande wake, Mfutakamba alielezea kushangazwa kwake kuhusu muda mrefu unaotumika katika na kuingiza vipuri hivyo.
Hata hivyo alitaka kuharakishwa kwa matengenezo ya kichwa hicho ili huduma za usafiri wa treni kwenda katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, zirejee.
Naibu waziri pia aliiagiza menejimenti ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), kushirikiana na viwanda vya ndani ya nchi vikiwemo vya Mang’ula na Mzinga, katika utengenezaji wa vipuri ili kuokoa muda na fedha.
Usafiri reli katika mikoa ya kanda ya ziwa, ulisitishwa na Kampuni ya Rites ya India iliyokuwa ikiendesha TRL tangu mwaka 2009 hadi mwishoni mwa mwaka jana baada ya serikali kuamua kuvunja mkataba.
0 Comments