Mwanaharakati wa masuala ya Jamii, John Daudi, ameiomba serikali kuwaangalia kwa karibu viongozi wa dini wanaotumia vibaya misamaha ya kodi wanayopewa ili kukomesha mtindo wa ukwepaji kodi.
Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipozungumza na waandishi wa habarI ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Daudi alisema viongozi wa dini wana dhamana kubwa katika jamii, lakini bahati mbaya hivi sasa wamejiingiza katika biashara kupitia misamaha ya kodi wanayopewa.
Alisema ana ushahidi wa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa matajiri kutokana na biashara wanazofanya bila kuzilipia kodi licha ya kutoa huduma ya kiroho.
Kutokana na baadhi ya madhehebu ya dini kutumia vibaya misamaha ya kodi wanayopewa na serikali, aliomba waondolewe na kutakiwa kulipa kila kitu wanachotaka kuingiza nchini kama ilivyo kwa wafanyabiashara wengine.
Aliongeza kuwa siku hizi watu wengi wanaibuka na kuanzisha makanisa chini ya miembe, lakini baada ya muda mfupi wanakuwa matajiri na kuhoji kuwa fedha hizo wanazipata wapi kwa kipindi kifupi.
0 Comments