Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 56 wa Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ukiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kutoka kulia ni Bibu Grace Mbwilo Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Bibi Kijakazi Mtengwa, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi Rahma Ali Khamis Mkurugenzi kutoka ZNZ, Mhe. Sophia Simba (Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Naibu Katibu Mkuu, Asha-Rose Migiro, Msajiri wa Mahakama ya Rufaa Bw. Francis Mtungi, Mhe. Zainabu Muhamed, Waziri wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mhe. Iman Daud Aboud Jaji wa Mahama ya Rufaa, Bibi Ellen Maduhu Afisa Ubalozi anayeshughulikia Kamati ya Tatu, Bibi Teodosia Mbunda Maendeleo ya Jamii na Bibi Joyce Mlowe kutoka Wizara ya Katiba na Sheria
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha- Rose Migiro akiwa na Mhe. Zainabu Omar Muhamed, Waziri wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mhe. Sophia Simba , Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto walipokaribishwa ofisini kwa Naibu Katibu Mkuu.
Mhe. Sophia Simba ( Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akichangia majadiliano kuhusu uwezeshwaji wa wanawake wa vijiijini katika siku ya kwanza ya mkutano wa 56 wa Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake. Mkutano huu ambao ni wa wiki mbili umefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha- Rose Migiro. Mada kuu ya mkutano huu ni nafasi ya wanawake wa vijijini na michango yao katika kupambana na umaskini na njaa, na jinsi gani ya kuwapatia uwezo ili kuwa kichocheo cha maendeleo endelevu. Aliyekaa nyuma na Waziri Simba ni Mhe. Zainabu Omar Muhamed. Waziri wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
NA Mwandishi Maalum
New York Mawaziri wanaohusika na masuala ya maendeleo ya wanawake kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, wameanza mkutano wao wa wiki mbili ambapo watajadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu hali ya wanawake hasa wale wa vijijini.
Mkutano huo ambao ni wa 56 umeandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake na umefunguliwa rasmi siku ya jumatatu na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha-Rozi Migiro hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani
Mada kuu ya mkutano huo ni “ nafasi ya wanawake wa vijijini na mchango wao katika kupambana na umaskini na njaa. Na namna gani wanaweza kuwezeshwa ili wapate nguvu ya kuwa kichocheo cha maendeleo endelevu”.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huu unaogozwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba ( Mb) akiwamo pia Mhe. Zainabu Omar Muhamed(Mb) Waziri wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, wanawake na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wengine waliomo katika ujumbe huo wa Tanzania, ni Bibi Kijakazi Mtengwa, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Iman Daud Aboud, Jaji Mahakama ya Rufaa, Bi Rahma Ali Khamis, Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Zanzibar, Bw. Francis Ali Khamis Mtungi, Msajiri wa Mahakama ya Rufaa.,Bibi Grace Job Mbwilo, | Page Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto , Bibi Joyce Mlowe kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Bibi Teodosia Mbuda, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Akifungua mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu ameeleza kwamba kama wanawake wa vijijini wangepewa fursa sawa ya kupewa nyenzo za uzalishaji, hapana shaka uzalishaji wa mazao ya kilimo ungeongezeka maradufu na kiwango cha njaa kingeshuka.
Hata hiyo anasema Migiro “ ukweli ni kwamba wanawake wa vijijini na wasichana wanaendelea kukabiliwa na vikwazo vingi vikiwamo ya upatikanaji wa ardhÃ, pembeje za kilimo, mitaji ya fedha , huduma na ugani na teknolojia za kisasa”
Na kuongeza kwamba, bado wanawake wa vijijini wanaendelea kukabiliwa na ugumu katika upatikanaji wa huduma za msingi zikiwano za ulizi wa jamii, ajira na masoko ya uhakika.
Na kwa sababu hiyo ametoa wito kwa wajumbe wa mkutano huo kujadiliana kwa kina kuhusu mikakati itakayowawezsha wanawake wa maeneo ya vijijini kuongeza uwezo wao wa kupambana na umaskini uliokithiri, njaa na kujiletea maendeleo endelevu katika familia zao.
Aidha Migiro anasema kwamba ili hayo yote yaweza kufanikiwa kwanza ni lazima jamii itambue kwamba wanawake ni mawakala muhimu wa mabadiliko. Na kwamba wakisaidiwa katika jumuia zao kutasaidia sana katika kuhakikisha kwamba ,matakwa na vipaumbele vya wanawake wa vijijini yanapewa umuhimu unaostahili.
“ Mkutano wa mwaka huu wa Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake, ni fursa nzuri ya kufikia maamuzi ya pamoja kati ya serikali na Asasi zisizo za kiserikali kuhusu mikakati ambayo kweli inaweza kuleta mabadiliko ya kweli kuhusu maisha ya wanawake wa vijijini “. Akasititiza Naibu Katibu Mkuu.
Kwa upande wake Waziri Sophia Simba akichangia majadiliano kuhusu hali ya wanawake wa vijijini, ameeleza kwamba, Tanzania licha ya kuweka será na sheria zinazolenga kumsaidia mwanamke pia imeanzisha benki ya wanawake inayolenga kumkomboa kiuchumi mwanamke akiwao yule wa kijijini.
Hata hivyo anasema ili será, na mipango iliyowekwa na serikali iweze kweli kumnufaisha mwanamke, ikiwamo mpango mkakati wa Kilimo Kwanza, bado suala la elimu ni muhimu sana kwa wanawake.
Akasema ni kwa kupitia elimu ndipo kweli mwanamke hasa yule wa kijijini kwanza, anaweza kujitambua yeyé ni nani lakini pia ataweza kuzitumia fursa anazo pewa kikamilifu.
Akatoa mfano kwa kusema kuwa katika kutambua umuhimu wa elimu si kwa wanawake tu, ndiyo maana serikali inaendelea kutekeleza upelekaji wa elimu ya msingi hadi ngazi ya kila kijiji na elimu ya sekondari kwa kila kata.
“ wanawake wakiwa na elimu watakuwa na uelewa mpana wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwamo za kudhulumiwa mali zao , lakini watakuwa na fursa ya kufahamu namna bora ya kutumia teknolojia za kisasa za kilimo, matumizi sahihi ya mitaji ya raslimali fedha na kubwa zaidi watajijengea uwezo mkubwa wa kupokea na kuzitumia kikamilifu na huduma mbalimbali zinazolengwa kuwainua na kukabiliana na mfumo dume ” akasisitiza Waziri Sophia Simba.
Kuhusu namna gani Umoja wa Mataifa unaweza kushirikiana na serikali katika kuchagiza maendeleo ya wanawake. Waziri Simba ametoa wito wa taasisi hiyo ya kimataifa, kuhakikisha kwamba inafanya kazi kwa karibu na serikali na kuzisaidia pale inapobidi kwa kusaidia uratibu na utekelezaji wa será, mipango na mikakati ambayo serikali inakuwa imejiwekea katika kuwakomboa na kuwaendeleza wanawake.
0 Comments