Kibaka alipoanza kusulubiwa na wananchi.
 Akakimbilia duka moja la mwanamke.
Wananchi wakiendelea kumsulubu.…
KIJANA mmoja anayesadikiwa kuwa kibaka, jana alinusurika kuuawa na wananchi baada ya kukamatwa akijaribu kuiba baiskeli katika eneo la nje ya benki ya NMB tawi la Wami katika Manispaa ya Morogoro.

Mtu huyo ambaye jina lake halikufahamika, aliepuka kifo baada ya kukimbilia kwenye duka moja la muuza dagaa ambaye aliwazuia wananchi wasimuulie hapo kwa kumfungia dukani humo.