Umoja wa Ulaya umetoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi wa kidemokrasia nchini Mali haraka iwezekanavyo kufuatia tukio la wanajeshi walioasi kumpindua rais Amadou Toumani Toure wa nchi hiyo.
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton (Pichani), amelaani mapinduzi hayo ikiwa ni pamoja na kusitishwa kwa shughuli za taasisi za umma nchini humo.
Asthon ametaka katiba irejeshwe tena na ufanyike uchaguzi ambao ulikuwa umepangwa kufanyika Aprili 29 mwaka huu.