MSANII kutoka katika kiwanda cha filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amesema kuwa, kufuatia sakata la kudaiwa kuzaa na msanii mwenzake Irene Uwoya, sasa analazimika kutafuta mganga ambaye atampatia dawa ya kumfanya asishobokewe na wanawake.
Dude aliyasema hayo hivi karibuni kutokana na kile alichodai kuwa, wanawake wengi wakiwemo wake za watu wanamshobokea kimapenzi kitu ambacho kinaweza kumtibulia.
Alisema kuwa, skendo ya kutuhumiwa kuzaa na Uwoya imempa fundisho hivyo ni vyema kujihadhari kabla hayajamkuta mengine.
“Niseme tu kwamba ishu ya Uwoya imenipa fundisho na kwa kweli niko tayari kutoa pesa yoyote kwa mganga yeyote ili anipe dawa ya kuniepusha na hawa wanawake kwani wananiletea matatizo hata kwenye maisha yangu na mchumba wangu,” alisema Dude.