Kijana Walid kulia na Maganga One. Walid ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 19 ni mkazi wa kitongoji kidogo cha Zaandam nchini Nederland.Kijana huyu anayesoma masomo ya biashara nchini humo ametokea kuupenda muziki tokea akiwa na umri mdogo sana.amekuwa na mapenzi na muziki kila siku zinavyozidi kwenda mbele na hajakata tamaa na kusema kwamba mziki ipo siku utamfikisha mbali sana kimaisha kutokana na kwamba anaujua vyema. Maganga One Blog ilimnasa kijana Walid katika moja ya show za muziki zilizokuwa zikifanywa jijini Amsterdam hivi karibuni.Walid kijana mcheshi mwenye kujiheshimu na kupenda watu hakusita kufanya mahojiano ya muda mfupi na Maganga One.mahojiano kati yetu siku hiyo yalikuwa kama ifuatavyo: Maganga One:Walid ebu tupe wasifu wako kiufupi Walid:Mimi ni kijana pekee katika familia yetu Maganga One:Shughuli hizi za muziki umeanza lini? Walid:nimeanza kazi za muziki toka nikiwa mdogo sana Maganga One:Nani hasa aliyekuvutia katika muziki? Walid:Kiukweli Michael Jackson ndiye aliyenivutia sana Maganga One:na msanii mwingine? Walid: msanii mwingine ni Brenda Fassie Maganga One:Nini hasa kilikuvutia kwa wasanii hawa? Walid: Uimbaji na uchezaji wao kiukweli nilivutiwa nao Maganga One:Walid unaishi na wazazi wako? Walid:Hapana Maganga One:Unaishi na nani na wapi? Walid: Ninaishi na bibi yangu mzaa baba na tunaishi Zaandam Maganga One:Ukiachilia mbali umaarufu ulionao kwenye muziki,je muziki unakulipa? Walid:Kiukweli mimi bado ni mchanga kwenye game ila nina imani utanilipa Maganga One:Nyimbo zipi ambazo zinatamba hivi sasa? Walid:nina nyimbo mbili kwa sasa ambazo zipo hot Maganga One: Unaweza kututajia ni nyimbo zipi? Walid:Nyimbo ya kwanza ni ``Your Down`` Maganga One:na ya pili? Walid:nyimbo ya pili ni This is WD Maganga One:Kwanini umeimba nyimbo zako kwa lugha ya Kiingereza? Walid:Ili mziki ufahamike kimataifa kwa haraka zaidi nimeona ni bora nitumie lugha hiyo Maganga One:Umejifunza wapi lugha ya Kiingerza? Walid:shuleni na mimi mwenyewe nakipenda thats Y Maganga One:Walid umesema unaishi na bibi,je wazazi wako wapo wapi? Walid:Wazazi wangu wote wapo Africa Maganga One:Walid ili watu waujue muziki wako wafanyeje? Walid:kuna link hii hapa inabidi waingie http://www.elijahrecords.nl/index.php/nieuws/82-mixtape-walid-gotta-b-love Maganga One:Ukiachilia muziki Walid nini unapenda Walid:Napenda sana ku Act Maganga One:Ukiwa na muda wa ziada Walid unapenda nini zaidi? Walid:Napenda sana kuchora,natumia muda wangu mwingi sana kwenye kuchora Maganga One:kwa Walid una kipaji zaidi ya kimoja sio? Walid:sawa kabisa Maganga One Maganga One:Muziki kwako ni kazi au starehe? Walid:muziki kwangu ni starehe na kwa upande mwingine ni kazi Maganga One:kazi zako za muziki unazifanyia wapi? Walid:kazi zangu nazifanyia SCAN music record Maganga One:Nani alikufundisha muziki? Walid:sikufundishwa na mtu ila nilikuwa napenda sana kuwaiga wanamuziki Maganga One:Kina nani hao? Walid:``snowman informer`` na ``Michael Jackson`` Maganga One:umetoa mixtape yako je inakwenda kwa jina gani? Walid:Gotta B love Maganga One:Una ujumbe wowote kwa wasanii wenzako au mashabiki wako? Walid:Yes,Ili ufanye mziki wako vyema inakubidi uusome mziki na kujituma zaidi,kwa mashabiki wangu nawapenda sana kwa sapoti zao na nawaahidi sitawaangusha. Maganga One:Walid nakushukuru sana kwa kutumia fursa hii kuwa nami chochote ukiwa nacho Maganga One Blog ni yako jihisi huru.. Walid:Ahsante sana Bro..!! JAMANI HII VIDEO HAPA CHINI NI KIJANA WALID NDIYE ALIYEIMBA HIYO NYIMBO YA ``YOUR DOWN`` KWA KWELI AMEFANYA KAZI NZURI SANA.KUNA NYIMBO NYINGINE NITAWAWEKEA BAADAE INAITWA ``THIS IS WD``. TUMPE SAPOTI KIJANA WETU. |
1 Comments